Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 08:52

Vipimo vyaonyesha waziri mkuu wa Finland hakutumia dawa za kulevya


Waziri mkuu wa Finland Sanna Marin akifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya video zinazomuonyesha akisherekea na marafiki zake kudukuliwa kwenye mitandao ya kijamii, Agosti 19, 2022. Picha ya Reuters.
Waziri mkuu wa Finland Sanna Marin akifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya video zinazomuonyesha akisherekea na marafiki zake kudukuliwa kwenye mitandao ya kijamii, Agosti 19, 2022. Picha ya Reuters.

Waziri mkuu wa Finland Sanna Marin hakuonekana kama alitumia dawa za kulevya katika kipimo cha matumizi ya dawa hizo alichofanya kufuatia kusambazwa mitandoni kwa kanda za video zikimuonyesha akisherekea na marafiki zake, ofisi ya waziri mkuu imesema Jumatatu.

Baadhi ya video za Marin, mwenye umri wa miaka 36, akiwa kwenye tafrija na watu wenye umaarufu wa Finland zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita na zikachapishwa kwa haraka na vyombo vya habari nchini Finland na nje ya nchi.

Alhamisi, Marin alisema amekasirishwa na kuona video akicheza muziki kwenye karamu za kibinafsi zinachapiswa mtandaoni na wakati zilikusudiwa kuonwa na marifiki zake pekee.

Marin, ambaye alikuwa kiongozi wa serikali mwenye umri mdogo duniani mwezi Disemba 2019, alikubali Ijumaa kufanya kipimo cha matumzi ya dawa za kulevya, akisema hajawahi kutumia hata siku moja dawa za kulevya na kwamba hakumuona yeyote akitumia dawa hizo kwenye karamu aliyohudhuria.

XS
SM
MD
LG