Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 13:12

Viongozi watuma rambi rambi Zambia


Frederick Chiluba, rais wa zamani wa Zambia akipiga kura katika uchaguzi wa nchi hiyo mwaka 2006
Frederick Chiluba, rais wa zamani wa Zambia akipiga kura katika uchaguzi wa nchi hiyo mwaka 2006

Chiluba alikuwa kiongozi wa kwanza Zambia kuchaguliwa katika mfumo wa demokrasia ya vyama vingi

Viongozi mbali mbali barani Afrika na kote duniani wanatuma salamu za rambi rambi Zambia kufuatia kifo cha rais wa zamani wa nchi hiyo Frederick chiluba. Msemaji wake alisema Bwana Chiluba alifariki nyumbani kwake Jumamosi mjini Lusaka baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na matatizo ya moyo na figo.

Bwana Chiluba aliiongoza Zambia kuanzia mwaka 1991 hadi 2002, akiwa ni kiongozi wa kwanza nchini humo kuchaguliwa kwa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Mtoto wa mchimba migodi na kiongozi wa wafanyakazi bw Chiluba alichukua uongozi wa Zambia baada ya karibu miaka 30 ya uongozi wa Kenneth Kaunda ambaye aliongoza nchi hiyo kutoka katika ukoloni.

Baada ya kuwacha uongozi Chiluba aliandamwa na madai kadha ya utumiaji mbaya wa mali ya umma wakati akiwa madarakani. Alikutwa na hatia ya kuiba mamillioni ya fedha za umma na mahakama moja ya London, lakini katika kesi nyingine ndani ya Zambia alikutwa hana hatia katika mashitaka mengine ya wizi wa dolla laki tano fedha za umma akiwa madarakani.

XS
SM
MD
LG