Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:54

Viongozi wa Sudan Kusini wafanya mazungumzo


Mpango wa kusitisha mapigano usioheshimiwa na viongozi wanaopingana nchini Sudan Kusini ulionekana kutekelezwa Jumanne.

Viongozi hao walipokutana mjini Juba baada ya mapigano ya siku nne yaliyosababisha vifo na maelfu kukimbia makazi.

Mazungumzo hayo yaliyoitishwa na rais Salva Kiir na mpinzani wake wa muda mrefu, makamu wa rais Riek Machar yalipokelewa vizuri na wananchi waliochoshwa na mapigano.

Vilevile serekali za nje zilifurahishwa pia kutokana na wasiwasi kwamba taifa hilo changa la Afrika linaweza kuingia katika vita kamili.

Washington, wizara ya mambo ya nje ilitoa tahadhari kwa msemaji wake John Kirby, kugusia mapigano ya kushtukiza katika sehemu za Juba licha ya kuwepo utululivu.

XS
SM
MD
LG