Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:41

Viongozi wa kimataifa watahudhuria mazishi ya Muhammad Ali


Mfalme Abdullah wa Jordan ni miongoni mwa watakaohudhuria mazishi ya Ali.
Mfalme Abdullah wa Jordan ni miongoni mwa watakaohudhuria mazishi ya Ali.

Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan na mfalme Abdullah wa Jordan watakuja Marekani kuhudhuria mazishi ya bingwa wa ndondi raia wa Marekani, Muhammad Ali baadae wiki hii, msemaji wa familia alisema.

Bob Gunnell alitangaza Jumatatu maelezo kuhusu mazishi ya Ali ambayo yanatarajiwa kufanyika katika makazi yake huko Louisville katika jimbo la Kentucky siku ya Ijumaa.

Dalai Lama alialikwa lakini alituma taarifa kwamba hatoweza kuhudhuria. Sala itajumuisha kumbukumbu ya umma katika ukumbi wa michezo ambao unahudumia watu 22,000.

Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan pia atahudhuria mazishi ya Ali.
Rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan pia atahudhuria mazishi ya Ali.

Shughuli hii itakuwa wazi kwa umma na kuoneshwa moja kwa moja kwa njia ya mtandao. Kutakuwepo pia na maandamano ambayo yatapita kote kwenye mitaa ya mji.

Siku ya alhamis itakuwa mazishi ya kifamilia pamoja na sala ya ki-Islam. Gunnell alisema maandalizi mengi ya mazishi yalipangwa na Ali mwenyewe kabla ya kifo chake kilichotokea Ijumaa iliyopita akiwa na umri wa miaka 74 kufuatia mapambano ya muda mrefu kwa ugonjwa wa Parkinson. Alisema kila kitu tunachofanywa hapa kilipewa baraka na Muhammad Ali na aliomba ifanyike hivyo.

XS
SM
MD
LG