Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:11

Viongozi wa IGAD wajadili mzozo wa Sudan Kusini


Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta (L) akiwa na viongozi wengine katika mkutano wa IGAD uliozungumzia mgogoro wa Sudan Kusini
Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta (L) akiwa na viongozi wengine katika mkutano wa IGAD uliozungumzia mgogoro wa Sudan Kusini
Kundi la kieneo barani Afrika linasema serikali ya Sudan Kusini imekubali kusitisha mapigano hatua ambayo itasaidia kumalizika kwa mapigano ya makabila mbali mbali ambayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1,000 mwezi huu.

Jumuiya ya nchi za pembe za Afrika- IGAD ilitangaza uamuzi huo mwishoni mwa mkutano uliofanyika ijumaa mjini Nairobi. Kundi hilo liliwasihi wafuasi wa Makamu Rais wa zamani, Riek Machar kufanya maamuzi kama hayo.

Mapigano yalianza huko Sudan Kusini mwanzoni mwa mwezi huu baada ya Rais Kiir alipomshutumu Machar kwa jaribio la mapinduzi.

Machar anasema ghasia zilikuwa matokeo ya ulipizaji kisasi wa mahasimu wa kisiasa wa bwana Kiir.

Ghasia hizo haraka ziliingia katika mtazamo wa kikabila huku wafuasi wa Rais Kiir wa kundi la kabila la Dinka wakipigana na kundi la wa-Nuer ambalo anatoka bwana Machar.

Katika mkutano wa Ijumaa, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alitoa wito kwa pande zote kufikia muafaka. “Tuna fursa ndogo sana kuhakikisha amani ambapo tunawasihi wadau wote kusitisha mapigano ikiwemo Riek Machar”.

Bwana Kenyatta anasema ghasia zinaweza kutishia uthabiti wa kieneo. “Kama ghasia za hivi sasa zinaendelea na ghasia za huko zinasababisha vifo dhidi ya raia, zitasababisha mgogoro wa kiulimwengu ambao itakuwa vigumu zaidi kwa sudan Kusini na eneo kufikia suluhisho”.

Rais Salva Kiir
Rais Salva Kiir
Awali Rais Kiir na Machar wote walisema walikuwa tayari kwa mashauriano lakini serikali ilikataa madai ya Machar kwamba viongozi wa upinzani waliofungwa kwanza waachiwe.

Ijumaa shirika la habari la Reuters lilisema majeshi ya serikali yaliwazidi nguvu wapiganaji wanaomtii Machar huko Malakal, mji mkuu wa jimbo la Upper Nile linalozalisha mafuta.

Alhamisi Umoja wa Mataifa ulisema ulitarajia kupeleka jeshi la walinda amani huko Sudan Kusini katika muda wa ndani ya saa 48.

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, Hilde Johnson alielezea umuhimu wa haraka wa kuongeza jeshi la Umoja wa mataifa. Alisema zaidi ya raia 50,000 walitafuta hifadhi ya kisiasa kwenye vituo vya Umoja wa Mataifa nchini humo tangu mapigano yalipozuka.Johnson aliwasihi viongozi wa kisiasa nchini humo kuzungumza na majeshi yao na kufanya kazi pamoja ili kuleta amani.
XS
SM
MD
LG