Hali hiyo imeongezeka katika siku za karibuni baada ya wa Venezuela kupiga kura ya maoni inayodai theluthi mbili ya eneo la Guyana.
Kutokana na shinikizo la viongozi wa kieneo, rais wa Guyana Irfaan Ali na mwenzake wa Venezuela Nicolas Maduro wamekubaliana kukutana kwenye uwanja wa kimataifa wa Argyle kwenye kisiwa hicho kilichoko mashariki mwa Caribbean cha St Vincent.
Mawaziri wakuu wa Barbados, Dominica na Trinidad and Tobago pia wamesema kwamba watahudhuria kikao hicho. Ali aliwasili kwanza akifuatiwa na Maduro, aliyezungumza na wanahabari kwanza kabla ya kuanza kwa kikao chao.
Forum