Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:37

Viongozi wa ECOWAS wanawahimiza wanajeshi kurudisha utawala wa kiraia Mali


Kanali Assimi Goita, kiongozi wa baraza la kijeshi Mali akihudhuria mkutano wa ECOWAS
Kanali Assimi Goita, kiongozi wa baraza la kijeshi Mali akihudhuria mkutano wa ECOWAS

Viongozi wa Jumuia ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS wamekutana mjini Accra, Ghana na mkuu wa baraza la kijeshi la Mali Jumanne, katika juhudi za kuwahimiza wanajeshi kurudisha utawala wa kiraia.

Marais wa nchi 15 za ECOWAS waliwapa viongozi wa kijeshi wa Mali hadi Septemba 15, 2020, ili kumtaja kiongozi mpya wa kiraia kuongoza utawala wa mpito nchini humo.

Rais Nana Akufo-Addo, rais wa Ghana akiongoza mazungumzo ya Mali mjini Accra
Rais Nana Akufo-Addo, rais wa Ghana akiongoza mazungumzo ya Mali mjini Accra

Kaimu mwenyekiti wa jumuia hiyo rais Nan Akufo-Addo wa Ghana, ammesema, "hii leo ndio ilibidi baraza la kijeshi kutangaza serikali ambayo itaambatana na masharti yaliyowekwa mwezi Ogusti. Jambo hilo halijatendeka."

Kiongozi wa Baraza la Kijeshi Kanali Assimi Goita, alihudhuria mkutano huo wa Accra, ikiwa ni mara yake ya kwanza kusafiri nje ya nchi tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Ogusti,

Baraza lake la kijeshi CSNP, mwishoni mwa wiki liliidhinisha mpango wa kuwepo na utawala wa mpito wa miezi 18 kwa ushirikiano na raia, lakini vuguvugu lililosababisha mapinduzi hayo la vyama vya upinzani, mashirika ya kiraia na kidini la M5-RFP limekata mapendekezo hayo.

Viongozi wa M5-RFP wanasema mapendekezo ya wanajeshi hayakutilia maanani hati ya mwisho walokubaliana na kwamba mazungumzo yalifanyika chini ya mazingira ya vitisho.

Vuguvugu hilo ndilo liliongoza maandamano tangu June 5 kumtaka rais Ibrahim Boubacar Keita, IBK, kuacha madaraka kutokana na ulaji rushwa ulokithiri, kushindwa kukabiliana na uwasi na ugaidi kaskazini mwa nchi pamoja na usimamizi mbaya wa utawala.

XS
SM
MD
LG