Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:39

Viongozi wa ECOWAS wakutana kujadili Niger


Viongozi wa Afrika Magharibi, wenye wasiwasi walipanga kukutana Jumamosi kwa mazungumzo kuhusu Niger, iliyokumbwa na mapinduzi na msururu wa migogoro ambayo imelitikisa eneo hilo.

Wakuu wa nchi wa jumuiya ya ECOWAS walikutana katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja, na walitarajiwa kujadili siasa na usalama nchini Niger pamoja na maendeleo ya hivi karibuni katika eneo hilo jumuiya imesema.

Rais wa Niger, Mohamed Bazoum, aliondolewa madarakani katika mapinduzi ya kijeshi Julai mwaka jana, na kusababisha ECOWAS kusimamisha biashara na kuweka vikwazo vikali.

Lakini onyo la jumuiya hiyo la kuingilia kijeshi limefifia na kuna dalili ndogo kwamba Bazoum, ambaye bado yuko kuzuizini katika ikulu ya rais mjini Niamey anakaribia kurejeshwa.

Katika kuelekea mkutano huo mawakili wa Bazoum waliitaka ECOWAS kushurutisha kuachiliwa kwake.

Forum

XS
SM
MD
LG