Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:11

Viongozi wa ECOWAS kuamua hatua mpya dhidi ya serikali za kijeshi za Afrika Magharibi


Viongozi wa ECOWAS wakutana Accra Ghana
Viongozi wa ECOWAS wakutana Accra Ghana

Viongozi wa jumuia ya maendeleo ya kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS wanakutana mjini Accra Ghana Jumamosi kwa lengo la kuzungumzia na kuamua ikiwa wapunguze au waongeze vikwazo dhidi ya utawala wa kijeshi nchini Mali, Burkina Faso na Guinea.

Viongozi hao wanatarajiwa kuamua ikiwa waendelee, wapunguze au waongeze vikwazo dhidi ya Mali vilivyowekwa mwezi Januari, baada ya utawala wa kijeshi kutangaza nia yake ya kuendelea kubaki madarakani kwa miaka mitano.

Rais Nana Akufo Ado akifungua mkutano huo amesema, nia yao ni kutafuta njia za kutathmini na kutafakari juu ya hali katika nchi hizo tatu na kutafuta njia za kuzisaidia kurudi kwenye utawala wa kikatiba chini ya raia.

Uanachama wa Guinea, Burkina Faso na Mali umesitishwa lakini ni Mali pekee iliyowekewa vikwazo, hadi sasa na hizo mbili huenda zikawekewa pia vikwazo baada ya viongozi wa nchi hizo kutangaza kwamba wataendelea kubaki madarakani.

ECOWAS ina dhamira ya kuzuia misukosuko ya kisiasa kuendelea kwenye kanda hiyo kwa viongozi kukutana na kuweka shinikizo kwa mabaraza ya kijeshi kupunguza muda wa kile wanachokieleza kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Lakini, Kanali Assimi Goita wa Mali, Kanali Mamady Doumbouya wa Guinea na Luteni Kanali Paul-Henri Sandago Damiba wa Burkina Faso wamepuuzi shinikizo kutangaza nia ya kubaki madarakani.

XS
SM
MD
LG