Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 06:19

Viongozi wa CHADEMA wakamatwa


Viongozi kadhaa wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA, walikamatwa na polisi Jumatatu kwa mahojiano, wakati wakifanya kikao cha ndani kilichokuwa kikifanyika katika hoteli ya Giraffe, jijini Dar es salaam.

Viongozi hao waliokamatwa ni Freeman Mbowe, Edward Lowassa, Dkt Vicent Mashinji, John Mnyika, na Said Issah, ambao walikuwa wakikutana na jumla ya wajumbe 170 wa chama hicho.

Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba walikuja watu waliodai kuwa ni polisi na kuzingira eneo la mkutano na kutaka viongozi hao kufika polisi kwa kukiuka agizo ambalo limakataza mikutano kama hiyo.

Kikao hicho kilikuwa ni cha kamati kuu ya CHADEMA na kinadaiwa kilikuwa kimeitwa kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya chama na kujumuisha wajumbe na wabunge wake.

Polisi waliwataka viongozi hao kufikishwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es salaam kwa mahojiano zaidi.

XS
SM
MD
LG