Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 17:41

Viongozi wa biashara Kenya waahidi kupambana na rushwa


Polisi wa barabarani Kenya akizuia matatu mjini Nairobi njia moja wapo ya kupata hongo.
Polisi wa barabarani Kenya akizuia matatu mjini Nairobi njia moja wapo ya kupata hongo.

Tume ya kupambana na ulaji rushwa nchini Kenya, KACC, imeombwa na muungano wa makampuni ya biashra, KEPSA kufanya uchunguzi na kutangaza makampuni ya kibinafsi yanayohusika katika ulaji rushwa.

KEPSA imesema, itafanyakazi pamoja na tume ya kupambana na rushwa kupiga vita ulaji rushwa katika sekta ya biashara binafsi nchini humo. Baada ya mazungumzo ya siku mbili taasisi hizo mbili zimetia saini hakti ya makubaliano ya kupambana na ulaji rushwa katika sekta ya biashara binafsi.

Akizungumza na Sauti ya Amerika mkurugenzi wa KACC PLO Lumumba, amesema wamekubaliana kushiriki pamoja kupambana na ufisadi. "Kile walichokiri ni kwamba kuna baadhi ya wanabiashara wanaofanya bishara na taasisi za umaa wanao jihusisha katika rushwa na kwamba ni lazima washirikiane nao ili kupiga vita rushwa kati yao wenyewe na kati yao na taasisi za umaa," amesema Lumumba.

Tatizo kubwa anasema, ni kwamba, kuna taasisi nyingi za umaa zinahitaji hongo kwanza kabla ya kutoa kandarasi, na ni jambo ambalo limekua likiendelea kwa muda mrefu."Wafanya biashara wamechoshwa na tabia hiyo kwa kua ni mzigo mkubwa kwao na ni mzigo ambao wananchi wanaubeba kutokana na kulipa bei za juu za bidha", amesema Lumumba.

Wafanyabishara wanasema wametambua kwamba bila ya kupiga vita tabia hii bishara zao zitaathirika zaidi katika siku za mbele na wawekezaji wengi hawana hamu ya kuwekeza huko Kenya, na jambo hilo litaumiza zaidi uchumi wa nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG