Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 10:38

Viongozi wa Ansar Dine wakamatwa Mali


Wapiganaji wa kundi la Ansar Dine wakiwa Timbuktu
Maafisa wawili waandamizi wa wanamgambo wa kislamu wamekamatwa huko kaskazini mwa Mali akiwemo kiongozi mmoja wa cheo cha juu wa kundi la ki-Islam lenye msimamo mkali la Ansar Dine.

Maafisa wa kundi la Wa Tuareg wanaotaka kujitenga kutoka Mali cha MNLA linasema liliwakamata Mohamed Moussa Ag Mohamed na Oumeini Ould Baba Akhmed siku ya jumamosi karibu na mpaka wa Mali na Algeria.

Ag Mohamed ni kiongozi wa tatu wa kundi la Ansar Dine na alisaidia katika utekelezaji wa sheria kali ya Ki-islam katika mji wa Timbuktu.

Baba Akhmed inaaminika kuwa mwanachama wa kundi la Movement for Unification and Jihad katika Afrika Mashariki lijulikanalo pia kama MUJAO.

Makundi hayo mawili pamoja na al-Qaida katika nchi za Afrika Maghreb walidhibiti miji mikubwa ya kaskazini mwa Mali kwa kiasi cha miezi tisa kabla ya kuondolewa na wanajeshi wa Ufaransa na Mali.

Ndege za kivita za Ufaransa ziliendelea kufanya mashambulia ya mabomu dhidi ya makundi ya ki-Islam siku ya Jumapili wakishambulia njia za kusafirisha vifaa na vituo vya kutoa mafunzo katika eneo la mbali katika jangwa la kaskazini-mashariki mwa Mali. Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius alisema lengo ni kuharibu kambi na ghala za wanamgambo, hivyo washindwe kuendelea kuwepo tena huko kaskazini mwa Mali.
XS
SM
MD
LG