Zaidi ya watu 200 wamefariki kutokana na dhoruba za vimbunga ambavyo vimepiga maeneo kadha ya kusini mwa Marekani katika muda wa siku mbili tatu zilizopita.
Sehemu kubwa ya maafa na vifo imetokea katika jimbo la Alabama ambako watu wapatao 149 wamekufa, ingawa Gavana Robert Bentley aliwaambia waandishi Alhamisi kuwa vifo vilivyothibitishwa ni kiasi cha 130.
Vimbunga vikali vilianza Jumanne usiku kuamikia Jumatano katika jimbo la Arkansas na maafa kuenea hadi jimbo jirani la Mississipi. Mfululizo wa vimbunga siku iliyopita uliuwa watu 10 Arkansas.
Maafisa katika jimbo la Texas wanasema vimbunga viliharibu nyumba karibu 100 Jumanne. Magavana wa Arkansas, Illinois, Indiana, Kentucky na Missouri wametangaza hali ya dharura kwa sababu ya tishio la mafuriko katika maeneo kadha ya majimbo hayo