Vimbunga vikali vilikumba eneo la mbali kusini mwa Marekani Ijumaa usiku, na kuua takriban watu 23 Mississippi, na kuhariibu majengo.
Pia vimeacha hali mbaya katika mji wa mashambani ambao meya alitangaza, mji haupo.
Idara ya kusimamia dharura ya Mississippi ilisema katika ujumbe wa Twitter kwamba timu za utafutaji na uokoaji kutoka kwa mashirika ya ndani na serikali zilitumwa kuwasaidia walioathiriwa na vimbunga.
Idara hiyo ilithibitisha Jumamosi watu 23 wamekufa, wanne hawajapatikana na kadhaa wamejeruhiwa.
Dakika chache baadaye, idara hiyo ilionya katika ujumbe wa Twitter kwamba idadi ya majeruhi inaweza kuongezeka.
Idara ya taifa ya hali ya hewa ilithibitisha kuwa kimbunga kilisababisha uharibifu takriban kilomita 96 kaskazini mashariki mwa Jackson, Mississippi.
Miji ya Silver City na Rolling Fork iliripoti uharibifu huku kimbunga kikisonga kaskazini mashariki kwa kasi yakilometa 113 kwa saa bila kupunguza kasi kuelekea Alabama pamoja na miji ya Winona na Amory, hadi usiku.