Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:28

Vikosi vya usalama Sudan vyafyatua mabomu ya machozi dhidi ya waandamanaji


Sudan
Sudan

Vikosi vya usalama vilifyatua mabomu ya machozi na maguruneti dhidi ya waandamanaji walioandamana dhidi ya watawala wa kijeshi wa Sudan siku ya Alhamisi, huku hatua za kidiplomasia za kutafuta suluhu  ya kisiasa katika mzozo wa baada ya mapinduzi zikionyesha dalili ndogo ya maendeleo.

Maelfu ya watu waliandamana kuelekea ikulu ya rais mjini Khartoum huku kukiwa na joto kali na kuwepo ulinzi mkali katika maandamano ya kwanza makubwa tangu mfungo wa mwezi wa Ramadhani na idadi kubwa ya watu waliojitokeza kupiga kura kwa wiki kadhaa.

Umati wa watu katika mji mkuu na wengine waliorekodiwa katika miji mingine kwenye mitandao ya kijamii walisikika wakiimba tuue, hatuogopi, na Serikali ya watu ni ya kiraia.

Sudan imekuwa katika msukosuko wa kisiasa tangu miezi kadhaa ya maandamano makubwa ambayo yalilisukuma jeshi kumpindua rais wa zamani Omar al-Bashir mnamo Aprili 2019.

XS
SM
MD
LG