Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 07:16

Vikosi vya Russia vimefanya mashambulizi ya anga kwa Ukraine


Mfano wa mashambulizi ya anga yanayofanywa huko Ukraine
Mfano wa mashambulizi ya anga yanayofanywa huko Ukraine

Maafisa wa Ukraine wamesema mashambulizi ya karibuni kutoka kwa makombora na silaha za Russia yaliupiga mji wa Druzhkivka mashariki mwa mkoa wa Donetsk pamoja na Kharkiv kaskazini mashariki mwa Ukraine na Dnipropetrovsk kusini mashariki mwa nchi hiyo

Vikosi vya Russia vilifanya mashambulizi ya anga katika maeneo kadhaa nchini Ukraine usiku wa kuamkia Jumanne huku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akionya kuwa Russia inaweza kuongeza matumizi yake ya ndege zisizo na rubani zilizotengenezwa na Iran.

Maafisa wa Ukraine wamesema Jumanne mashambulizi ya karibuni kutoka kwa makombora na silaha za Russia yaliupiga mji wa Druzhkivka mashariki mwa mkoa wa Donetsk pamoja na Kharkiv kaskazini mashariki mwa Ukraine na Dnipropetrovsk kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Zelenskyy alisema wakati wa hotuba yake kwa njia ya video Jumatatu usiku kwamba serikali yake ina taarifa kwamba Russia inapanga "shambulio la muda mrefu" na ndege zisizo na rubani za Shahed ambazo imetumia katika miezi ya karibuni kufanya mashambulizi katika maeneo kote Ukraine.

Zelenskyy amesema Russia inaweza kubashiri "uchovu wa watu wetu, ulinzi wetu wa anga, sekta yetu ya nishati" huku akiwapongeza wale wanaohusika katika kuilinda Ukraine dhidi ya mashambulizi ya angani.

XS
SM
MD
LG