Kituo cha kijesi cha Marekani kilisema mapema Jumamosi kwamba vikosi vyake vilishambulia kombora la majini ambalo kilisema lilikuwa katika eneo linaloshikiliwa na Wahouthi na lililenga Bahari ya Sham na ambalo lilikuwa tayari kurushwa.
Katika chapisho kwenye mtandao wa X, CENTCOM ilisema kuwa vikosi vya Marekani viliharibu kombora hilo kwa kujilinda baada ya kuamua kwamba kombora katika maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi nchini Yemen lilikuwa tishio la karibu kwa meli za wafanyabiashara na meli za Jeshi la Wanamaji la Marekani katika eneo hilo.
Mapema Ijumaa, meli ya kijeshi ya Marekani USS Carney ililengwa na kombora la Wahouthi ilipokuwa likishika doria katika Ghuba ya Aden. Waliangusha kombora hilo, lakini ilikuwa mara ya kwanza kwa meli ya kivita ya Marekani kulengwa na waasi hao wenye makao yao huko Yemen.
Forum