Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 04:46

Vikosi vya kikurdi vyapanua operesheni Syria


Wapiganaji wa Kiarabu wa Syria wakipata mafunzo ya kutumia silaha.
Wapiganaji wa Kiarabu wa Syria wakipata mafunzo ya kutumia silaha.

Vikosi vya kikurdi vinavyoungwa mkono na Marekani vimepanua operesheni zake magharibi mwa Syria katika mto wa Euphrates.

Vikosi vya kikurdi vinavyoungwa mkono na Marekani vimepanua operesheni zake magharibi mwa Syria katika mto wa Euphrates, unaokatisha eneo la hatari la Uturuki. Hili ni jambo ambalo limepandisha hasira kwa waasi wa kiarabu wa madhehebu ya Sunni.

Watetezi wa kisiasa wanaonya kwamba hatua hiyo inahatarisha mapigano kaskazini mwa Syria, na kwamba ghasia kadri saa zinavyoendelea huenda zikasababisha waarabu wa kisuni kuishia mikononi mwa kundi la kigaidi la Islamic State.

Wapinzani wakubwa wa kisiasa wa Rais Assad wa Syria sasa wanataka kuhakikishiwa na jumuiya ya kimataifa kwamba waarabu wa kisuni wataruhusiwa kurudi katika vijiji vilivyoshikiliwa na kundi la Islamic State na vilivyokombolewa na vikosi vya Syrian Democratic ambavyo vinaundwa na vikosi vya 'Kurdish People’s Protection' ama YPG.

XS
SM
MD
LG