Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:02

Vijana wengi wa Iran wasubiri kunyongwa


Kundi mashuhuri la kimataifa la kutetea haki za binadamu lilieleza kwamba idadi kubwa ya vijana huko Iran wanasubiri kwa muda kutekelezwa adhabu ya kifo kwa uhalifu walioufanya walipokua na umri chini ya miaka 18.

Hiyo ikiwa ni chini ya sheria ambayo inaruhusu wasichana wenye umri wa miaka 9 na wavulana wenye umri wa miaka 15 kunyongwa.

Amnesty International Logo
Amnesty International Logo

Amnesty International, kundi lenye makao yake mjini London katika ripoti iliyopewa jina “Growing Up on Death Row: The Death Penalty and Juvenile Offenders in Iran”,iliishutumu Iran kwa kutojali haki za watoto ikiwa moja wapo ya taifa la mwisho duniani lenye kuwahukumu kifo vijana.

Ripoti hiyo imetaja kuorodhesha kunyongwa kwa vijana 73 huko Iran kati ya mwaka 2005 na mwaka 2015 huku ikinukuu takwimu za Umoja wa Mataifa zikionesha angalau wahalifu 160 vijana hivi sasa wanasubiri utekelezwaji wa adhabu yao ya kifo.

XS
SM
MD
LG