Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 16:53

Vijana waaswa kuingia katika kilimo Tanzania


Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete akionyeshwa mapapai yaliolimwa kitaa,lam na Adam Ngamange mwanzilishi wa mtandao wa kijani kibichi Tanzania nyumbani kwake Msoga mkoani Pwani.
Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete akionyeshwa mapapai yaliolimwa kitaa,lam na Adam Ngamange mwanzilishi wa mtandao wa kijani kibichi Tanzania nyumbani kwake Msoga mkoani Pwani.

Mtandao wa Mkikita au mtandao wa kijani kibichi Tanzania unaelenga kufanya mageuzi ya kilimo nchini humo .

Mwanzilishi wa mtanbndao huo Adam Ngamange ambaye ni mtalaam wa uhasibu aliyeacha kazi hiyo na kuingia katika kilimo alizungumza na Jukwaa la Vijana la VOA na kusema kilimo kinaanzia kwenye ubongo wa mtu au akilini mwa mlimaji mwenyewe halafu baadaye ndio kinaingia mkononi.

Mjasiriamali huyo anasema kilimo ni fikra pana na kwenye mtandao wao wanataka kubadili fikra za watanzania katika mtazamo huo ambao sasa unaungwa mkono na watanzania wengi nchini humo aliongeza.

Kwa upande wa mapinduzi ya kilimo na teknolojia wanasisitiza kuwepo masoko na nini kifanyike kukidhi masoko ya ndani na nje ya nchi hiyo wakiangalia usalama wa chakula na ubora wa masoko.

Ngamange anasisitiza kilimo hai nchini humo ni kujaribu kuhakikisha ardhi hiyo inakuwa bora kwa miaka 100 ijayo.

Mtandao huo unamiliki mashamba kadhaa wakifanya utafiti wa bidhaa za kilimo masoko na maeneo ya kupata mashamba.

Jambo jingine ni kusaidia na kulea wakulima wadogo wadogo na mashamba na kuunganisha wasomi,walaji na wakulima wa maeneo mbali mbali.

Wana mashamba ya block huko katika maeneo ya Vikindu, Ruaha na Kibaha na mashamba ya mtu mmoja mmoja katika mikoa ya Tanga , Pwani, Mbeya na Njombe wakiwa wanasaidia wakulima zaidi ya 6,000 kupata masoko na mitaji ya kufanyia kazi zao ikiwa ni pamoja na Bima na masuala mazima ya teknolojia na wataalam.

Kwa hiyo kwa jumla mtandao huu naunganisha walaji, watumiaji na wazalishaji.

Wanatoa huduma kwa kutumia whatsapp, vipindi vya TV , blog yao ya living GreenTz.com na mikutano mbali mbali kupitia vikundi na taasisi mbali mbali kuweza kuwasaidia wakulima wadogo wadogo.

XS
SM
MD
LG