Shirika la uangalizi wa haki za binadamu la Syria lenye makao yake nchini Uingereza lilisema, Jumamosi kwamba shambulio la Marekani lilisababisha vifo vya watu 19, kutoka 14 walioripotiwa hapo awali.
Rais wa Marekani Joe Biden, alisema Marekani itajibu kwa nguvu kuwalinda Wamarekani baada ya jeshi la Marekani kusema lilifanya mashambulizi ya anga mashariki mwa Syria kujibu shambulio linaloshukiwa kuungwa mkono na Iran.
Akizungumza katika ziara ya kitaifa nchini Canada siku ya Ijumaa, rais Biden alisema Marekani haitafuti mzozo na Iran lakini iko tayari kuchukua hatua za nguvu kuwalinda watu wake.