Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 22:13

Vifo vya watoto Gambia vyahusishwa na dawa ya kikohozi-WHO


Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, alipowasili katika mkutano wa CHOGM mjini Kigali. REUTERS.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, alipowasili katika mkutano wa CHOGM mjini Kigali. REUTERS.

Vifo vya darzeni ya watoto nchini Gambia kutokana na majeraha ya figo vinaweza kuhusishwa na dawa za kikohozi zilizoingia uchafu ambazo  zilitengenezwa na mtengenezaji mmoja wa madawa wa India, Shirika la Afya Ulimwenguni lilisema Jumatano.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwaambia waandishi wa habari kwamba shirika la Umoja wa Mataifa linachunguza pamoja na wadhibiti wa India na mtengenezaji wa dawa, Maiden Pharmaceuticals yenye makao yake mjini New Delhi.

Maiden Ilikataa kutoa maoni yake kuhusu tahadhari hiyo, huku simu na ujumbe wa maandishi wa Reuters kwa Mdhibiti Mkuu wa Dawa nchini India zikiita bila kujibiwa. Gambia na wizara ya afya ya India pia hazikujibu mara moja ombi la kutoa maoni.

WHO pia ilitoa tahadhari ya bidhaa za matibabu ikiwataka wadhibiti kuondoa bidhaa za Maiden Pharmaceuticals kwenye masoko.

XS
SM
MD
LG