Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 01:43

Vifo kutokana na shambulizi la jumanne Somalia vimeongezeka


Wakazi wa Somalia wakikusanyika kwenye eneo lilipotokea shambulizi

Maafisa wa Somalia wanasema idadi ya vifo kutokana na bomu lililotegwa kwenye gari jumanne karibu na makazi ya rais imeongezeka kufikia vifo visivyopungua 22 baada ya majeruhi kadhaa kufariki kutokana na majeraha waliyoyapata.

Gari liligonga ukuta wa hoteli ya SYL, eneo maarufu la mikutano kwa maafisa wa serikali ya Somalia. Mkuu wa kitengo cha gari la kubeba wagonjwa katika eneo, Dr.Abdulkadir Aden, anasema kitengo chake kilisafirisha maiti 22 na majeruhi 30 baada ya mlipuko. Miongoni mwa watu hao waliokufa sita walikuwa wanawake.

Afisa wa polisi mjini Mogadishu, Meja Mohamed Abdullah aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba watu 50 walijeruhiwa katika shambulizi hilo. Miongoni mwa waliojeruhiwa katika mlipuko huo walikuwa waziri wa usafiri, waziri wa ulinzi, wabunge kadhaa na waandishi wa habari wawili wa redio kutoka kwenye eneo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG