Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 22:27

Vifo kutokana na mafuriko ya Ufilipino vyafikia 13, huku watu 23 wakiendelea kutafutwa


Timu za waokozi kwenye mafuriko ya Ufilipino
Timu za waokozi kwenye mafuriko ya Ufilipino

Idadi ya vifo kutokana na mvua kubwa zilizonyesha wakati wa Krismasi kusini mwa Ufilipino imeongezeka hadi 13, wakati mamlaka zikisema Jumanne kwamba watu 23 wanaendelea kutafutwa , huku viwango vya maji kutokana na mafuriko vikiendelea kupungua.

Idara ya dharura imesema kwamba vifo vingi vilisababishwa na mafuriko baada ya mvua za siku mbili kuvuruga sherehe za Krismasi, na kupelekea zaidi ya wakazi 45,000 kuchukua hifadhi kwenye vituo maalum.

Picha kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha timu za uokozi zikiwasaidia wakazi waliokwama kwenye mafuriko, huku baadhi ya barabara zikiwa zimefungwa kutokana na hali hiyo.

Carmelito Heray anayeongoza timu ya dharura kwenye mji wa Clarin uliopo jimbo la Misamis Occidental ameiambia radio ya DZBB kwamba operesheni za uokozi zinaendelea wakati pia wakikadiria hasara iliyokea kwenye sekta ya kilimo.

Mifugo kama vile ng’ombe, mbuzi na kuku wanasemekana kuangamia pia kutokana na mafuriko.

XS
SM
MD
LG