Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 22:07

Vibali vya wafanyakazi kutoka Zimbabwe vyaongezwa muda na mahakama Afrika Kusini


Watu wakiwa kwenye mpaka wa Beitbridge karibu na mji wa Musina, kati ya Afrika Kusini na Zimbabwe.
Watu wakiwa kwenye mpaka wa Beitbridge karibu na mji wa Musina, kati ya Afrika Kusini na Zimbabwe.

Mahakama moja ya Afrika Kusini Jumatano imetoa hukumu dhidi ya serikali na kuamuru kwamba ibatilishe uamuzi wake wa kusitisha vibali maalum vilivyoruhusu karibu raia laki 2 wa Zimbabwe kuishi na kufanya kazi nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, hatua hiyo ingelazimisha watu hao kurejea makwao Zimbabwe iwapo hawangepata vibali vya kuendelea kufanya kazi, licha ya kwamba baadhi wana watoto waliozaliwa Afrika Kusini, na ambao ni raia halali wa taifa hilo.

Mahakama kuu ya Gauteng mjini Pretoria imesema kwamba uamuzi wa wizara ya masuala ya ndani wa 2022 wa kusitisha vibali maalum kwa raia wa taifa jirani la Zimbabwe ulikuwa kinyume cha sheria pamoja na katiba, na wala haukufuata mikakati ya mashauriano.

Vibali hivyo sasa vimeongezwa muda wake hadi Juni 28 mwaka ujao kufuatia hatua ya mahakama. Awali, tarehe ya mwisho iliyokuwa imewekwa ilikuwa Juni 30 mwaka huu. Takriban raia 178,000 wa Zimbabwe sasa hivi wanaishi na kufanya kazi Afrika Kusini chini ya mpango huo.

Forum

XS
SM
MD
LG