Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 01:41

Uzoefu wa kijana aliyelelewa katika familia ya rangi tofauti


Familia ikiwalelea watoto wa rangi tofauti

Angela Tucker ambaye katika ukuaji wake alikuwa akijihisi hajakamilika, hata akiwa ndani ya familia kubwa ya ndugu saba, baadhi yao wazungu, baadhi weusi, wengi wao wamechukuliwa kulelewa.

Alipokuwa na umri wa miaka 26, amegundua kuwa mama yake mzazi, alimsaidia kujihisi kuwa amekamilika, amesema.

Hivi sasa akiwa na miaka 33, anasaidia katika huduma za watu wanaotaka watoto wa kuwalea huko Seattle katika ofisi ya Amara, anazungumzia yeye kama mmoja wa waliolelewa na kuwasaidia watoto wadogo kujijenga na kujifahamu vyema.

Tucker kuwatafuta wazazi waliomzaa alipata msaada mkubwa kutoka kwa watu waliomlea Teresa na David Burt.“Ilikuwa vgumu sana kwangu mimi kwanza, kwasababu nilihisi pengine yeye kukutana na mama yake mzazi ingekuwa kama vile anatafuta mtu mzazi mbadala,” Teresa Burt alisema.

Lakini 2anasema mtoto wake alimbadilisha mawazo yake, nakumuwezesha kuwa sehemu ya hiyo azma ya kutaka kumuona mama mzazi na ilikuwa ni hamasa kubwa. Kwa kweli ilinifanya nijisikie niko huru.

”David Burt anasema hakuhisi chochote, hakuwa na khofu kwamba azma ya Angela huenda ingedumaza uhusiano wake na mtoto wake wa kike.

‘’Nilipata furaha ya kumlea tangu alipokuwa na umri wa mwaka mmoja mpaka alipongia chuoni. Sikupoteza chochote,” amesema.Tucker alimpata baba yake mzazi kwanza na halafu mama yake mzazi, Deborah takriban, muongo mmoja uliopita.

Anazungumzia na kuwasiliana naye mara kwa mara.Deborah anasema kuwasiliana na mwanawe ilikuwa ni kama “zawadi kutoka kwa Mungu.”

Tucker bado hana majibu kwa maswali yote anayomuuliza Deborah. Mwanamke kijana anakiri kwamba tofauti za maisha ikiwa ni pamoja na fursa ya elimu nzuri na kiuchumi juu ya Deborah ni kikwazo.

“hivyo, anadhani kwamba mawasiliano ni magumu kutokana na hilo.”Yeye na Deborah wanapendana, na mawasiliano ya karibu, lakini wanaishi kitofauti kabisa,” amesema Tucker.3

Teresa Burt anasema mtoto wake kumtafuta mzazi wake kumemfanya kuwa na nguvu zaidi. Baada ya kufanya hivyo, anaweza kuwasaidia wengine na hivi sasa anaisaidia wengine kutafuta wazazi wao.”

Tucker amefungua tovuti ambayo inazungumzia yale aliyoyapitia na kuweka mfululizo wa visa kwa msaadawa mume wake ambaye ni mtengenezaji filamu, Bryan Tucker.

Humo kuna makala inayoitwa “The Adopted Life” kwenye http://www.theadoptedife.com/episodesAnazungumza ana kwa ana na vijana ambao wanalelewa na walezi, na kutumia ujuzi wake huko Amara, ambao ameanza kuwaingiza katika program maalum ya ushauri.

Mmoja wa wale ambao wanalelewa na walezi ambao si wazazi wao kibaiolojia ni Maggie, ana umri wa miaka 9 ni mtoto wa Amy na Brett Bowton-Meade. Wawili hao, ambao ni wazungu, pia wana watoto wawili wa kike ambao ni wa kuwazaa.Maggie amekuwa akijitahidi kujibu maswali kuhusu anahusika wapi na mama yake mzazi yuko wapi.

Tucker, mshauri wake, amemtia moyo kuweka rekodi ya kila kitu.“Nimekuwa nikiandika kila kitu katika kitabu change,” Maggie amesema, akielezea kwamba kitabu hicho pia kina picha. “Kama nitakutana naye siku yoyote, nitakwenda nacho.”

4Akiwa kazini, Tucker anajaribu kurahisisha utaratibu wa kuasili watoto, ikiwemo kusukuma mawazo kama vile kuzishawishi familia za watu weusi nao kuchukua watoto kuwalea.“Sisemi kwamba kuasili kuwe tu kwa watu rangi fulani. Lakini ninachosema ni kama vile unatembea katika mstari mwembamba sana,” amesema.Tangu awapate wazazi wake, Tucker anasema anahisi, “Hana mkanganyiko ten. Lakini ukweli ni kwamba mama yake mzazi hakuweza kumlea ni jambo la kusikitisha. Na hilo halitabadilika.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG