Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 18:06

Uzalishaji wa mafuta wasitishwa Libya kutokana na maandamano


Sehemu ya kuhifadhi mafuta ya Brega nchini Libya
Sehemu ya kuhifadhi mafuta ya Brega nchini Libya

Shirika la taifa la Mafuta la Libya, limesema kwamba maandamano makubwa nchini humo yameathiri uzalishaji wa mafuta na huenda sekta hiyo ikaathirika zaidi.

Makundi manne yamesitisha uzalishaji wa mafuta kote Libya.

Waandamanaji wanamtaka Waziri mkuu wa Tripoli Abdul Hamid Dbeibah kukabidhi madaraka kwa serikali hasimu inayoongozwa na Fathi Bashaga, iliyoundwa mwezi uliopita.

Serikali hizo mbili zimekuwa zikishindana kuchukua madaraka tangu bunge la Libya lilipomteua Bashaga kuwa Waziri mkuu.

Lakini Dbeibah amesema kwamba bado ana mamlaka ya kuongoza taifa hilo hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika mwezi June.

XS
SM
MD
LG