Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:45

Uturuki yakumbwa na tetemeko jingine


Waokoaji wakitafuta walionusurika katika jengo la hoteli mashariki mwa Uturuki jumatano.
Waokoaji wakitafuta walionusurika katika jengo la hoteli mashariki mwa Uturuki jumatano.

Uturuki yakumbwa na tetemeko jingine la ukubwa wa 5.7 vipimo vya rikta

Tetemeko la 5.7 kwenye vipimo vya rikta lilikumba eneo la mashariki mwa Uturuki Jumatano usiku na kuuwa watu wapatao watatu na kupromosha majengo yapatayo 20.

Dazeni ya watu inaaminika wamenaswa katika vifusi katika eneo la Van karibu na mpaka wa Iran.Watu wapatao 10 walionusurika wamefukuliwa chini ya majengo yalioanguka mpaka sasa.

Tetemeko hilo limetokea chini ya wiki 3 baada ya tetemeko linguine la ardhi kukumba Uturuki katika eneo hilo kuuwa watu wapatao 600 na maelfu kadhaa kupoteza makazi yao.

XS
SM
MD
LG