Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 08:22

Uturuki ya saini mikataba tisa na Tanzania


 Rais Recep Tayyip Erdogan akihutubia waandishi i wa habari Tanzania.
Rais Recep Tayyip Erdogan akihutubia waandishi i wa habari Tanzania.

RAIS wa Uturuki Recep Tayip Erdogan akiw akatika ziara rasmi nchini Tanzania leo Jumtatu amesaini mikataba tisa ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Rais huyo ametahadharisha nchi za kiafrika juu ya kuwepo kwa mtandao wa Fethullah Gulen uliofanya jaribio la mapinduzi nchini Uturuki mwezi Julai mwaka jana.
Katika mkutano wa pamoja na Rais John Magufuli amewaambia waandishi wa habari umuhimu wa kukuza kiwango cha biashara baina ya Tanzania na Uturuki kutoka dola za kimarekani milioni 150 hivi sasa hadi kufikia dola za kimarekani milioni 500. Rais Erdogan aliwasili nchini Jumapili, akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili.

Sera ya Uturuki Afrika

Rais Erdogan amesema sera ya uturuki kuhusu Afrika imejikita katika kunufaisha pande zote mbili.

Rais huyo aliongeza kusema serikali yake inafuta njia bora ya kuleta maendeleo na kuliunganisha bara la Afrika huku akisema Uturuki kama mwanachama wa Taasisi ya Kiislam (OIC) ni ya pili katika nchi zilizo piga hatua kiuchumi.

Kuhusu mtandao wa Fethullah, rais huyo wa Uturuki amesema wanachama wa kiongozi huyo wameenea kila mahali hivyo ni muhimu kwa nchi mbalimbali kuchukua tahadhari.

Hata hivyo alisita kuzungumzia uwepo wa mtandao wa shule zinazodaiwa za wanachama hao za FEZA zilizopo nchini humo.

Uongozi wa shule hizo za FEZA nchini Tanzania katika taarifa maalum wakati wa vuguvugu la mapinduzi hayo ilikanusha kuhusika na mtandao huo wa Fethullah.

Rais John Magufuli
Rais John Magufuli

Kwa upande wake mwenyeji wake rais Magufuli alizungumzia mikakati mbalimbali ya ukuaji wa uchumi inayotekelezwa na serikali yake hivi sasa akigusia maombi ya mkopo kutoka Benki ya Exim ya Uturuki. Amesema tayari ameshawasilisha kwenye mazungumzo yake na rais Erdogan mradi wa kujenga sehemu ya kilometa 400 ya reli ya Standard Gauge (SGR) licha ya kwamba moja ya makampuni ya Uturuki yanawania zabuni katika ujenzi wa reli hiyo itakayounganisha nchi ambazo hazina bandari.

Kwa upande wake waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na waziri wa Afya, Ummy Mwalimu wamezungumzia mikataba waliyosaini leo katika sekta za utalii na afya.

Mikataba mingine iliyosainiwa ni kati ya mashirika ya ndege ya Tanzania na Uturuki, mashirika ya utangazaji ya nchi hizo mbili, mkataba wa maendeleo baina ya Tanzania na Uturuki, Mkataba wa ushrikiano katika sekta ya elimu na utafiti, mkataba kati ya shirika la kuendeleza viwanda vidogo Tanzania SIDO na shirika la kuendeleza viwanda vya kati Uturuki, mkataba wa ushirikiano katika viwanda vya ulinzi na mkataba wa ushirikiano baina ya chuo cha diploamsia cha Tanzania na Chuo cha Diplomasia cha Uturuki.

Rais huyo amefuatana na mkewe mama Emine Erdogan pamoja na mawaziri watatu ambao ni waziri wa Mambo ya Nje, Mevlüt Çavuşoğlu, waziri wa Uchumi, Nihat Zeybekekci na waziri wa Nishati na Maliasili, Berat Albayrak

Rais pia amefuatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.Taarifa ya ziara yake imeonyesha kutakuwa pia na kongamano la kibiashara litakalo waleta pamoja wafanyabiashara wa pande zote mbili Tanzania na Uturuki.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Dina Chahali, Tanzania

XS
SM
MD
LG