Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 20:18

Utoaji mimba watatiza wa-Repuplican


M-Mrepuplican Todd Akin aliyetoa matamshi yenye utata kuhusu "ubakaji halali" akiwa na mkewe eneo la Sedalia, Missouri
M-Mrepuplican Todd Akin aliyetoa matamshi yenye utata kuhusu "ubakaji halali" akiwa na mkewe eneo la Sedalia, Missouri

Romney anaepuka suala lililogawanyika la utoaji mimba na kulenga kwenye uchumi katika jaribio la kumshinda Obama katika uchaguzi mkuu Novemba.

Wademocrat wanajaribu kutumia kwa faida yao matamshi yenye utata ya mgombea Mrepuplican katika kiti cha baraza la Seneti kuhusu utoaji mimba lakini mgombea urais kupitia chama cha Repuplican Mitt Romney anajaribu kurejesha mjadala wa kampeni yake katika swala la kudorora kwa uchumi.

Mbunge Todd Akin wa chama cha Repuplican ambaye anagombea nafasi ya kiti kwenye baraza la Seneti katika jimbo la Missouri, alianza kujibu mashambulizi wiki hii wakati alipojitetea kuhusu msimamo wake kwenye suala la utoaji mimba hata katika kesi ya ubakaji kwa kudai kwamba waathirika wa “ubakaji halali” wana mifumo ya kiasili mwilini kuepuka ujauzito. Akin baadae aliomba radhi lakini alikataa wito uliotolewa na viongozi wa Repuplican akiwemo Romney kujitoa katika kinyang’anyiro cha nafasi ya kiti katika baraza la Seneti.

Rais Barack Obama alikejeli matamshi ya Akin wakati wa hafla ya uchangishaji fedha kwenye chakula cha jioni huko New York, jumatano usiku. Alisema kuwa japokuwa Akin ni mjumbe wa kamati ya bunge ya teknolojia, “kwa kiasi fulani alipitwa na darasa la ufahamu wa sayansi”.

Kwa upande wa chama chake Romney anajaribu kuepuka suala lililogawanyika la utoaji mimba na kulenga kwenye uchumi katika jaribio lake la kumshinda bwana Obama katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba. Akifanya kampeni katika jimbo la Iowa, Romney alimkosoa bwana Obama kwa kushindwa kumaliza deni na nakisi ya taifa. Alisema kama akichaguliwa atakata matumizi ya serikali kuu na kuhamasisha ukuaji na kwamba matokeo yatakuwa sawa na bajeti ya serikali kuu.
XS
SM
MD
LG