Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:42

Utawala wa kijeshi Burkina Faso umetoa kibali cha uchimbaji madini kwa Russia


Mfano wa eneo la mgodi wa madini ulioko huko Hounde, Burkina Faso, Feb. 13, 2020.
Mfano wa eneo la mgodi wa madini ulioko huko Hounde, Burkina Faso, Feb. 13, 2020.

Nordgold tayari inatumia migodi mitatu ya dhahabu kupitia matawi mawili ya ndani kaskazini mwa Burkina Faso eneo ambalo limekumbwa na ghasia za wanajihadi tangu mwaka 2015.Kampuni hiyo ya Russia ilifunga mgodi wa Taparko kwa sababu za kiusalama mwezi April

Utawala wa kijeshi unaoshikilia madaraka nchini Burkina Faso umetoa kibali cha uchimbaji wa mgodi mpya wa dhahabu kwa kampuni ya Russia ya Nordgold serikali imesema Alhamisi.

Kibali cha miaka minne katika eneo la Yimiougou katikati mwa nchi kitaruhusu uzalishaji wa jumla ya tani 2.5 za dhahabu, serikali imesema.

Pato katika mgodi huo litaleta dola milioni 8.5 kwa bajeti ya serikali na na kkasi kingine cha fedha kitakwenda kwenye mfuko wa maendeleo ya madini nchini.

Nordgold tayari inatumia migodi mitatu ya dhahabu kupitia matawi mawili ya ndani kaskazini mwa Burkina Faso, eneo ambalo limekumbwa na ghasia za wanajihadi tangu mwaka 2015.

Kampuni hiyo ya Russia ilifunga mgodi wa Taparko kwa sababu za kiusalama mwezi Aprili.

Dhahabu ni mauzo ya juu ya Burkina Faso kabla ya pamba.

Russia inapata uungwaji mkono mkubwa miongoni mwa mataifa ya Afrika yanayozungumza Kifaransa huku nguvu ya zamani ya kikoloni Ufaransa ikikashifiwa.

Maandamano yanayoiunga mkono Russia yamekuwa yakifanyika nchini Burkina Faso tangu mapinduzi ya kijeshi yalipofanyika Septemba 30.

XS
SM
MD
LG