Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 20:16

Utawala wa Hamas unadai mashambulizi ya Israel yameua zaidi ya watu 90 Gaza


Moshi ukifuka angani huko Kusini mwa Ukanda wa Gaza wakati wa mashambulizi ya Israel. Picha na AFP
Moshi ukifuka angani huko Kusini mwa Ukanda wa Gaza wakati wa mashambulizi ya Israel. Picha na AFP

Mashambulizi ya Israel yameua zaidi ya watu 90 usiku kucha, wizara ya afya chini ya utawala wa Hamas huko Gaza imesema leo Alhamisi.

Mashambulizi hayo mapya yamefanyika huku dawa kwa ajili ya mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo na msaada mpya kwa raia ukiingia katika eneo la Palestina chini ya makubaliano mapya ya hivi karibuni, Qatar ambaye ni mpatanishi imesema.

Wizara ya afya huko Gaza imesema watu 93 waliuawa, wakiwemo 16 waliouawa katika shambulio moja kwenye nyumba katika mji wa kusini wa Rafah, ambako watu wengi walikimbilia.

“Shambulio hilo limeua watu 16, miongoni mwao wanawake na watoto, na wengine 20 walijeruhiwa,” wizara hiyo imesema.

Israel imesema mashambulizi yake yamewalenga wanamgambo wa Hamas kaskazini na kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israel linasema limeua wanamgambo 40 katika eneo la Khan Younis kusini mwa Gaza, na wengine kadhaa waliuawa katika mashambulizi ya anga na ardhini kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Mapigano yameuteketeza Ukanda wa Gaza tangu Hamas ilipofanya mashambulizi yasiyokuwa ya kawaida ndani ya Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana, mashambulizi ambayo yaliua watu 1,140, wengi wao wakiwa raia, kulingana na taarifa zilizokusanywa na shirika la habari la AFP kwa kunuku takwimu rasmi za Israel.

Forum

XS
SM
MD
LG