Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:33

Utawala wa Burkina Faso wadaiwa kulazimisha wakosoaji kujiunga kwenye vita dhidi ya wanamgambo


Kiongozi wa Burkina Faso Ibrahim Traore kwenye picha maktaba.
Kiongozi wa Burkina Faso Ibrahim Traore kwenye picha maktaba.

Utawala wa kijeshi wa Burkina Faso inatumia vibaya sheria ya dharura kuandikisha wanaodhaniwa kuwa wapinzani na wakosoaji wake kuijiunga kwenye vita hatari dhidi ya wanamgambo.

Watu hao wanasemekana kulazimishwa kupambana na watu wanaohusishwa na makundi ya kigaidi ya Al Qaida na Islamic State, mawakili, wanahabari pamoja na kundi la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch wamesema wiki hii.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, makundi hayo yanalaumu utawala wa kijeshi kwa kujaribu kunyamazisha uasi wa amani wakati ukijitahidi kurejesha hali ya usalama, kama ulivyoahidi wakati wa kuchukua madaraka kupitia mapinduzi ya Septemba 2022.

Mmoja wa wanachama wa shirika la wanahabari ambaye hakutaka kutambulishwa ameambia Reuters kwamba “ tumeanza kuona uso kamili wa utawala wa kijeshi, kwamba haujakuja kuokoa Burkina Faso.” Msemaji wa utawala huo hajajibu madai hayo hata baada ya kuombwa kufanya hivyo.

Forum

XS
SM
MD
LG