Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 22:43

Utawala wa Biden wasisitiza kuwepo kanuni zaidi za serikali kuu kuweka mtandao  salama


Rais wa Marekani Joe Biden akiongea na vyombo vya habari baada ya kuhudhuria chakula cha mchana cha Baraza la Seneti la Democratic Caucus katika Ikulu ya Marekani huko Washington, D.C., Marekani, Machi 2, 2023. REUTERS
Rais wa Marekani Joe Biden akiongea na vyombo vya habari baada ya kuhudhuria chakula cha mchana cha Baraza la Seneti la Democratic Caucus katika Ikulu ya Marekani huko Washington, D.C., Marekani, Machi 2, 2023. REUTERS

Utawala wa rais Biden unasisitiza kuwepo kwa kanuni za kina zaidi za serikali kuu ili kuweka eneo la mtandaoni kuwa  salama dhidi ya wavamizi,

Hii ikiwa ni pamoja na kuhamisha majukumu ya usalama wa mtandao kutoka kwa watumiaji hadi kwa wadau wa tasnia na kuchukulia mashambulizi ya mtandao kama vitisho vya usalama wa kitaifa.

Mpango huo ni sehemu ya Mkakati wa Kitaifa wa Mtandao ambao utawala ulitoa siku ya Alhamisi, ukionyesha malengo ya muda mrefu ya jinsi watu binafsi, serikali na wafanyabiashara wanaweza kufanya kazi kwa usalama katika ulimwengu wa kidigitali.

Hii ni pamoja na kuweka uwajibikaji kwenye sekta ya kompyuta na programu ili kutengeneza bidhaa zilizo salama kwa muundo ambao zimeundwa kimakusudi, kutengenezwa na kujaribiwa ili kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya dosari zinazoweza kutumiwa kabla ya kuingizwa sokoni.

Mkakati huo kimsingi unafikiria upya mkataba wa kijamii wa mtandao wa Marekani na utasawazisha tena jukumu la kudhibiti hatari ya mtandao kwa wale ambao wanaweza kustahimili, Kaimu Mkurugenzi wa Kitaifa wa Mtandao Kemba Walden alisema Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari kuhakiki mkakati huo.

XS
SM
MD
LG