Utawala wa Biden unachukua hatua kushughulikia hatari za kiuchumi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ikitoa ripoti ya kurasa 40 leo Ijumaa juu ya mipango ya serikali ya kulinda masoko ya fedha, bima, na nyumba, na kuziokoa familia za kimarekani.
Chini ya repoti hiyo mchakato wa rehani, ufichuzi wa soko la hisa, mipango ya kustaafu, na bajeti ya serikali yote yanazingatiwa ili nchi iweze kuwa na bei katika hatari zinazotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Ripoti hiyo ni ufuatiliaji wa amri ya kiutendaji ya mwezi Mei iliyotolewa na Rais Joe Biden ambayo kimsingi inatoa wito kwa serikali kuchambua namna joto kali, mafuriko, dhoruba, moto wa msituni na kufanya marekebisho mapana ya kushughulikia mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanaweza kuathiri uchumi mkubwa zaidi duniani.
Ikiwa mwaka huu umetuonyesha chochote, ni kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yanaleta hatari inayoendelea, na ya kimfumo kwa uchumi wetu na kwa maisha ya wamarekani ya kila siku, na lazima tuchukue hatua hivi sasa, Gina McCarthy, mshauri wa White House wa hali ya hewa kitaifa aliwaambia waandishi wa habari.