Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 18:11

Utawala wa Biden kutoa vipimo milioni 500 vya nyumbani katika mapambano ya covid


Rais Biden aliposaini mpango wa kuwanusuru wamarekani ambao ni wa kiuchumi kupambana na janga la covid 19. White House mjini Washington, Marchi 11, 2021. REUTERS/Tom Brenner
Rais Biden aliposaini mpango wa kuwanusuru wamarekani ambao ni wa kiuchumi kupambana na janga la covid 19. White House mjini Washington, Marchi 11, 2021. REUTERS/Tom Brenner

Utawala wa Biden utafungua maeneo ya upimaji COVID-19 katika Jiji la New York wiki hii na kununua vifaa vya vipimo vya haraka milioni 500 vya  nyumbani ambavyo Wamarekani wanaweza kuagiza kwa njia ya mtandao bila malipo

Utawala wa Biden utafungua maeneo ya upimaji COVID-19 katika Jiji la New York wiki hii na kununua vifaa vya vipimo vya haraka milioni 500 vya nyumbani ambavyo Wamarekani wanaweza kuagiza kwa njia ya mtandao bila malipo kuanzia Januari inapojaribu kukabiliana na aina mpya ya Omicron inayoenea nchini.

Katika maelezo juu ya hali ilivyo mbaya ambayo anatarajiwa kutoa katika hotuba yake leo kuhusu hatari za kutopokea chanjo, Rais Joe Biden ataweka wazi mipango hiyo yenye lengo la kuwashawishi Wamarekani kujikinga na aina hiyo inayoenea kwa kasi sana, afisa mkuu wa utawala alisema.

Hatua hizo ni pamoja na kuwaita wanajeshi 1,000 wa afya kusaidia katika hospitali.

Pia tutaeleza kwamba ikiwa hujachanjwa, uko katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa, aina hii ya virusi inaambukiza sana na wale ambao hawajachanjwa wana uwezekano wa kulazwa hospitalini mara nane zaidi na uwezekano wa kufa kutokana na COVID ni mara 14 zaidi, afisa huyo alisema.

XS
SM
MD
LG