Ingawa hiyo huenda ikawa habari njema, ina maana kwamba kuna plastiki nyingi zilizopo ndani ya bahari, utafiti huo umeongeza. Ripoti hiyo imesema pia kwamba uchafu wa plastiki unaofika baharini ni mdogo mara 10, chini ya viwango vilivyokisiwa na wanasayansi hapo nyuma.
Kwa kutumia utaalam wa komputa wa 3D kuchukua takwimu kwenye fukwe, juu na ndani ya bahari, watafiti wanakisia kuwa huenda kuna takriban tani nusu milioni za plastiki zinazoingia baharini kila mwaka.
Mapema mwaka huu, taasisi ya Five Gyres, yenye makao yake makuu katika jimbo la California, hapa Marekani, na inayoshughulikia kupunguza uchafuzi wa plastiki, ilichapisha utafiti ukionyesha viwango sawa vya plastiki kwenye bahari kama vilivyotolewa na ripoti hiyo.
Forum