Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 10:51

Usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine unaendelea licha ya Russia kujiondoa kwenye makubaliano


Meli zilizobeba nafaka kutoka Ukrainian zikiwa katika bahari ya Black Sea, huku Russia ikiendelea kushambulia Ukraine, karibu na bandari ya Odesa, Ukraine, Okt 30, 2022
Meli zilizobeba nafaka kutoka Ukrainian zikiwa katika bahari ya Black Sea, huku Russia ikiendelea kushambulia Ukraine, karibu na bandari ya Odesa, Ukraine, Okt 30, 2022

Meli tatu zaidi zimeondoka bandari za Ukraine Jumanne adhuhuri zikiwa zimebeba nafaka, ikiwa ni siku ya pili baada ya Russia kujiondoa kwenye makubaliano ya usafirishahi wa nafaka na ngano katika bahari ya Black Sea.

Kituo cha uratibu kinachoongozwa na Umoja wa Mataifa kimesema kwamba meli hizo zimeondoka Ukraine kwa kuzingatia makubaliano kati ya serikali ya Ukraine, Uturuki na Umoja wa Mataifa, na kwamba Russia imepewa taarifa kuhusu usafiri wake.

Makubaliano ya kusafirisha chakula kutoka bandari za Ukraine, yalipatikana kufuatia mazungumzo yaliyosimamiwa na Uturuki na Umoja wa Mataifa mwezi Julai.

Russia ilikuwa imezuia usafirishaji wa nafaka na ngano kutoka Ukraine na kupelekea uhaba mkubwa wa bidhaa hizo katika soko la kimataifa.

Meli 12 ziliondoka Ukraine Jumatatu.

Rais wa Russia Vladimir Putin amesema kwamba hatua ya Russia ya kujiondoa katika makubaliano hayo inatokana na shambulizi la ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya meli za Russia huko Crimea, lililotokea Jumamosi. Russia imedai kwamba Ukraine ndio ilitekeleza shambulizi hilo.

Ukraine haijasema iwapo ilihusika na shambulizi hilo na imefutilia mbali madai ya kutumia njia ya kusafirisha nafaka iliyokubaliwa katika mkataba, kwa sababu za kijeshi.

Waziri wa ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar, amemwambia waziri wa ulinzi wa Ukraine kwamba kuendelea kutekeleza makubaliano ya kusafirisha nafaka na ngano ni muhimu sana, na kwamba mpango wa kibinadamu unastahili kuheshimiwa katika vita vya Ukraine.

XS
SM
MD
LG