Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 12:17

Marekani na Saudia waahidi mshikamano kujibu njama za Iran


Mlango mkuu wa ubalozi wa Saudi Arabia mjini Washington DC, October 11,2011
Mlango mkuu wa ubalozi wa Saudi Arabia mjini Washington DC, October 11,2011

Marekani na Saudi Arabia wameahidi mshikamano kujibu njama za Iran za kutaka kumuuwa balozi wa saudia mjini Washington

Marekani na Saudi Arabia wameahidi kufanya kazi kwa bidii na ushirikiano wa kimataifa kujibu njama inazodaiwa zilizofanywa na serikali ya Iran kumuuwa balozi wa Saudi Arabia Adel al-Jubeir mjini Washington, Marekani.

White House ilisema Rais wa Marekani Barack Obama na Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia walizungumza kwa njia ya simu Jumatano na walikubaliana kuwa njama hizo zinawasilisha ukiukwaji wa maadili ya kanuni za kimataifa na waliapa kuwawajibisha wale wanaohusika na vitendo hivyo.

Iran inakanusha shutuma hizo. Shirika la habari la serikali-IRNA lilimkariri naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran, Ali Ahani, Jumatano akiliita tukio hilo ni la kutisha na kuisihi Saudi Arabia kuwa makini na juhudi za Marekani za kuharibu uhusiano wa nchi katika eneo hilo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton alisema njama zinatishia kuongezeka hatari iliyotumika muda mrefu katika ghasia za kisiasa na ufadhili wa ugaidi nchini Iran. Alisema Marekani itafanya kazi kwa karibu na marafiki zake wa kimataifa kuongeza kiwango cha kutengwa cha Iran na kutia msukumo katika serikali yake.

Majibu hayo makali yamekuja siku moja baada ya wizara ya sheria ya marekani kutangaza ilimfungulia mashtaka Manssor Arbabsiar, raia wa Marekani mwenye asili ya Iran na Gholam Shakuru, mwanachama wa kikosi maalum cha jeshi nchini Iran, kwa kupanga njama za kufanya shambulizi moja la bomu kwa balozi wa Saudi Arabia.

Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Eric Holder, alisema njama zilipangwa, kufadhiliwa na kuongozwa kutoka Iran.

XS
SM
MD
LG