Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 00:22

Wabunge wa Marekani wazungumzia Libya


Seneta Lindsey Graham(L), Seneta John McCain(C) na seneta Joe Lieberman(R) wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Kabul nchini Afghanistan, Julai 3, 2011
Seneta Lindsey Graham(L), Seneta John McCain(C) na seneta Joe Lieberman(R) wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Kabul nchini Afghanistan, Julai 3, 2011

Wabunge wa ngazi ya juu hapa Marekani Lindsey Graham na Joe Liberman wanamuhimiza Rais Barack Obama kuwaelezea wa-Marekani na bunge msimamo halisi wa kile Marekani inataraji kupata kutoka Libya.

Seneta Liberman alisema ikiwa Rais Obama ataeleza malengo ya Marekani kwa ufasaha zaidi huenda kukawa na uungaji mkono zaidi wa bunge katika kuhusika kwa Marekani kwenye kampeni ya kijeshi inayoogozwa na NATO huko Libya.

Wabunge wa chama cha Republican na wale wa chama cha Demokrat wamekasirishwa na Rais Obama kwa kutoomba idhini ya bunge katika kuingia kwenye kampeni za Nato nchini Libya.

Mwezi uliopita hamasa hizo zilijitokeza wazi katika kura mbili kwenye baraza la wawakilishi lenye wanachama wengi wa Republican. Kura moja ilikuwa ni kutoa idhini ya kuhusika kwa majeshi ya Marekani huko Libya, na nyingine ni ya kukata kugharamia operesheni hizo za kijeshi.Hatua zote hazikufanikiwa. Lakini kura nyingine juu ya Libya inatarajiwa kufanyika Jumanne.

Ghasia za kutaka Rais Ghadafi aondoke madarakani na kumaliza miongo minne ya utawala wake zimeendelea kwa miezi mitano sasa na bado hakujapatikana suluhisho. Nchi za magharibi zimewaunga mkono waasi katika kumtaka Ghadafi aondoke madarakani na wamechangia katika mashambulizi ya angani ya NATO dhidi ya vikosi vinavyomuunga mkono Ghadafi.


XS
SM
MD
LG