Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:24

Trump na Sanders wanyakua ushindi wa uchaguzi wa awali huko Indiana


Mgombea wa chama cha republican, Donald Trump
Mgombea wa chama cha republican, Donald Trump

Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump ashinda katika uchaguzi wa jimbo la Indiana hio jana, hatua ilosababisha mpinzani wake mkubwa Ted Cruz, kuamua kujitoa katika mbio hizo. Kwa upande wa Demokrat, mgombea Bernie Sanders afanikiwa kumshinda Bi Hillary Clinton katika jimbo hilo la Indiana.

Bw Trump alipata asli mia 53.2 za kura, naye Cruz alifanikiwa kupata asli mia 36.7 za kura. Akizungumza baada ya uchaguzi akiwa mjini Louisville Kentucky, Bw Sanders alisema kuwa, Hillay Clinton anadahani kampeni hii imemalizika. Lakini wamekosea. Hata hivyo licha ya kushindwa huko Indiana, Bi Clinton hadi sasa ana wajumbe asli mia 92 wanaohitajika kunyakuwa nafasi ya kuwa mgombea kwa tiketi ya chama cha Demokrat.

XS
SM
MD
LG