Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:24

Walinzi wa pwani ya Marekani wameidhinisha juhudi mpya za BP

Walinzi wa pwani ya Marekani wameidhinisha mpango wa karibuni wa shirika la mafuta la Uingereza BP wa kuzuia mafuta yanayomwagika katika ghuba ya Mexico kutoka kwenye kisima kilichopo katika pwani hiyo.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano mkuu wa walinzi wa eneo la mbele la pwani hiyo Admiral Mary Landry amesema baada ya majadiliano na wanasayansi wa serikali amethibitisha kile kinachoitwa operesheni ya juu ya BP.

Mpango huo umehusika kwenye kusukuma udongo uliochanganyika na taka nzito za majihadi kwenye kisima ili kuzuia mafuta yanayomwagika ambayo imekuwa vigumu kuyazuia.

Wafanyakazi wa BP katika juhudi za kusaka kifaa cha kuzuia umwagikaji mafuta.
Wafanyakazi wa BP katika juhudi za kusaka kifaa cha kuzuia umwagikaji mafuta.

Haijafahamika bado lini kampuni hiyo itaanza mpango huo. Kampuni hiyo iliwahi kusema ilikuwa inafanya kwanza majaribio ili kujua kama mpango huo utafanyakazi ipasavyo.

Ikulu ya Marekani imesema Rais Barack Obama atakuwa na mkutano na waandishi wa habari alhamis kujadili tatizo hilo la kumwagika mafuta na taratibu mpya zinazoathiri viwanda vya mafuta katika pwani.

Msemaji wa Rais Obama anasema Rais atajibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari siku moja kabla ya yeye mwenyewe kurejea katika eneo hilo la ghuba Ijumaa ijayo.

XS
SM
MD
LG