Huku karibu nusu ya kura zote zikiwa zimehesabiwa, rais wa Zambia Edgar Lungu alionekana kuongoza kwa kura chache kufikia siku ya Jumapili, huku upinzani ukitoa wito wa kutaka matokeo ya uchaguzi yatangazwe kwa haraka zaidi kukiwa na kuhofia ya wizai wa kura.
Kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo ECZ, Lungu anaongoza akiwa na kura mia 679,960 dhidi ya mpinzani wake, mwenye kura 645,132, kutoka wilaya 156 za uchaguzi.
Rais huyo wa sasa anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Hakainde Hichilema, wa chama cha UPND ambaye amekuwa akumshutumu kwamba ameshindwa kuliongoza taifa hilo kutoka kwa uchumi uliodorora, na ongezeko la bei za bidhaa, licha ya kuwa kwa nafasi ya pili barani Afrika kwa utoaji wa madini ya shaba nyekundu.
Facebook Forum