Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 13:07

Upinzani washinda uchaguzi Ushelisheli


Seychelles-vote-POLITICS
Seychelles-vote-POLITICS

Mgombea wa upinzani ameshinda uchaguzi nchini Ushelisheli kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1977.

Baada ya kutangazwa mshindi, Wavel Ramkalawan ameahidi kupandisha kima cha chini cha mshahara baada ya janga la covid 19 kuathiri uchumi wa taifa hilo linalotegemea sana utali.

IKulu ya Ushelisheli imesema katika taarifa kwamba Ramkalawan na makamu wake Ahmed Afif wataapishwa leo.

Ramkalawan, ambae ni kasisi wa zamani wa kanisa la Anglican alimshinda rais Danny Faure baada ya kuwania urais bila maafanikio kwa miongo mitatu.

Ramkalawan alipata asilimia 54 ya kura naye rais Faure alipata asilimia 43.5 katika uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, tume ya uchaguzi imesema.

Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG