Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Uganda Dr. Kizza Besigye amesema yeye na chama chake cha FDC wanafanya maandalizi kujitokeza pekee katika kinyang’anyiro cha urais mwaka ujao kama hakutakuwa na mabadiliko katika muungano wa Democratic Alliance.
Hili linafuatia mzozo ulioibuka ndani ya muungano huo baada ya kumchagua waziri mkuu wa zamani Amama Mbabazi kama mgombea wake atakayekabiliana na rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi wa mwaka 2016.
Mfuasi wa bwana mbambazi , Mao Nobert amesema wiki iliyopita kwamba muungano huo wa vyama hauwezi kufikia makubaoliano ya mwisho kwa sababu Kiza Besyige hajakubali uteuzi wao.
Wafuasi wa besigye wanaona umaarufu wake unaweza kumwingiza madarakani kwa urahisi.
Lakini wachambuzi wanaona mgawanyiko huu ndani ya muungano wa vyama vya upinzani nchini Uganda unaweza kuhamasisha ushindi kwa rais Yoweri Museveni mwaka ujao.