Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 05:32

Upinzani wa Venezuela unapinga matokeo ya uchaguzi


Kaimu rais wa Venezuela Nicolas Maduro akiwapungia mkono wafuasi wake baada ya kupiga kura mjini Caracas, Venezuela, Jumapili, Apr. 14, 2013.
Kaimu rais wa Venezuela Nicolas Maduro akiwapungia mkono wafuasi wake baada ya kupiga kura mjini Caracas, Venezuela, Jumapili, Apr. 14, 2013.
Tume huru ya uchaguzi ya Venezuela imemtangaza kaimu rais Nicolas Maduro kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais kwa kura milioni 7.5 ikiwa sawa na 50.7%, akimshinda mpinzani wake Henrique Capriles aliyepata kura milioni 7.3, ikiwa sawa na asili mia 49.1 kufuatana na matokeo ya awali.

Maduro aliyeshinda kwa idadi ndogo alikiri kulikuwepo na kasoro kwenye uchaguzi lakini alitowa wito kwa upinzani kufanya kazi pamoja kuijenga nchi akisema, "tunafahamu kwamba kuna sehemu ya upinzani ambao hautatambua matokeo ambayo nimeshinda kwa kura laki tatu."

Wachambuzi wengi walitabiri kwamba Maduro atapataushindi mkubwa zaidi hasa kwa vile alichaguliwa na kiongozi mashuhuri aliyemtangulia Hugo Chavez aliyefariki mwezi uliyopita kutokana na ugonjwa wa saratani.

Wachambuzi wanasema ushindi wake mdogo unasababisha nchi kugawika na atakuwa na kazi kubwa ya kuiunganisha tena taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.

Kiongozi wa upinzani Capriles anasema hatakubali matokeo hadi kura kuhesabiwa tena kwani anasema kura zilizohesabiwa na kampoeni yake ni tofauti na matokeo ya tume ya uchaguzi.
XS
SM
MD
LG