Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 17:49

Upinzani wa Comoros walalamikia uchaguzi wa Jumapili


Rais wa sasa wa Comoros Azari Assoumani anayetarajiwa kushinda tena kwenye uchaguzi wa Jumapili
Rais wa sasa wa Comoros Azari Assoumani anayetarajiwa kushinda tena kwenye uchaguzi wa Jumapili

Uchaguzi wa Comoros imefanyika Jumapili, ukitarajiwa kutoa ushindi kwa wa muhula wa nne wa miaka 5 kwa Rais Azari Assoumani.

Uchaguzi huo imefanyika wakati wapinzani wake watano wakidai ulijawa na udanganyifu, na kwamba baadhi ya masanduku ya kupigia kura tayari yalikuwa yamejazwa kura za kumchagua Assoumani.

Zoezi la upigaji kura lilianza kwenye visiwa hivyo vya bahari Hindi saa 2 za usubuhi, likishirikisha wapiga kura 338,940 waliojiandikisha kati ya jumla ya wakazi 800,000 nchini humo.

Upigaji kura ulimalizika saa 12 za jioni kwenye taifa hilo ambalo limeshuhudia takriban majaribio 20 ya mapinduzi, tangu kupata uhuru wake kutoka ka Ufaransa mwaka 1975.

Baadhi ya viongozi wa upinzani wanadai kuwa tume ya uchaguzi inapendelea chama tawala, suala ambalo imekanusha na kusema kwamba zoezi hiyo litakuwa lenye uwazi.

Forum

XS
SM
MD
LG