Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 23:08

Upinzani unapinga jeshi kuchukua madaraka Burkina Faso


Kiongozi wa upinzani Jean Hubert Bazie (kati kati) anasoma taarifa akiwa na kiongozi wa upinzani Burkina Faso Zephirin Diabre (kulia), akisisitiza wanapinga jeshi kuiongoza nchi.

Vyama vya upinzani na mashirika yasio ya kiserikali ya Burkina Faso yameitisha maandamano makubwa Jumapili ili kupinga uwamuzi wa jeshi kuchukua uwongozi wa serikali ya mpito.

Mkuu wa majeshi Jenerali Nabere Honare Traore, alitangaza Jumamosi kwamba, baraza la wakuu wa majeshi kwa sauti mmoja limemteuwa luteni kanali Isac Yacouba Zida kuongoza serikali ya mpito kwa mwaka moja.

Katika taarifa aliyotowa ameeleza kwamba luteni kanali Zida atakutana na viongozi wa upinzani na wa mashirika ya kiraia kwa mashauriano juu ya kuunda serikali ya mpito.

Uwamuzi huo haujawaridhisha viongozi hao wa upinzani na wakiraia kwani kufuatana na katiba ya Burkina Faso, pindi rais atakapoacha madaraka rais wa bunge la taifa anabidi kuchukua nafasi yake kwa muda hadi kuitishwa uchaguzi mwengine wa rais.

Hatua hiyo hitowezekana, kutokana na uwamuzi ulochukuliwa na wakuu wa jeshi kulivunja bunge na kusitisha katiba ya nchi. Viongozi wa upinzani wanashikilia kwamba ni lazima kwa serikali ya mpito kuongozwa na raia.

Wakati huo huo Rais Aliassane Outara wa Ivory Coast ametangaza kwamba serikali yake imempokea rasmi Bw. Compaore, familia yake, na washauri wake wa karibu.

Taarifa yake inaeleza kwamba taifa hilo jirani linawasi wasi kutokana na hali inayoendelea huko Burkina Faso na kuwatakia wananchi wake kuchukua hatua za busara zitakazo dumisha amani na utulivu.

XS
SM
MD
LG