Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 07:39

Upinzani nchini Uganda wasisitiza kupinga matokeo

Kiongozi wa upinzani wa Uganda Kizza Besigye akiwa amekamatwa na polisi
Kiongozi wa upinzani wa Uganda Kizza Besigye akiwa amekamatwa na polisi

Sheria ya uchaguzi ya Uganda inatoa siku 10 za kuasilisha malalamishi kuanzia siku ya kutangazwa matokeo.

Chama kiku cha upinzani nchini Uganda kimesema kinafanya kila kiwezalo kutafuta ushahidi utakaopelekea kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Februari 18.

Sheria ya uchaguzi ya Uganda inatoa siku 10 za kuasilisha malalamishi kuanzia siku ya kutangazwa matokeo.

polisi wa uganda wakizuiya waandishi wa habari kupiga picha
polisi wa uganda wakizuiya waandishi wa habari kupiga picha

Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha FDC Mugisha Muntu amesema chama chake kinafanya kila juhudi ili kuwasilisha ushahidi kabla ya wakati uliowekwa kumalizika.

Hata hivyo ameongeza kuwa kumekuwa na dhuluma na ukandamizaji kutoka kwenye vyombo vya usalama vya serikali ikiwemo idara ya polisi.

Muntu ameyasema haya kufuatia kukamatwa mara kadhaa kwa Dkt Kizza Besigye aliekuwa mgombea urais wa chama cha FDC.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Badru Kiggundu alimtangaza rais Yoweri Museveni kuwa mshindi kwa kujipatia asilimia 60.07 ya kura zilizopigwa huku Besigye akifuatia kwa asilimia 35.37 za kura.

XS
SM
MD
LG