Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:44

Upinzani Zambia kuwasilisha malalamishi kortini Ijumaa

Tume ya uchaguzi ya Zambia ilimtangaza Edgar Lungu kama mshindi wa uchaguzi wa rais kwa kupata asili mia 50.35 ya kura zote zilizopigwa, huku mpinzani wake Hakainde Hichilema, akipata asili mia 47.67 ya kura.

Chama kikuuu cha upinzani cha Zambia, UPND, kina mipango ya kuwasilisha malalamishi katika mahakama ya kikatiba hapo kesho Ijumaa, kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika tarehe kumi na moja mwezi huu ambao ulimpa rais wa sasa Edgar Lungu ushindi.

Chama hicho pia kinadhamiria kuzuia kutawazwa kwa bwana Lungu sherehe zilizopangwa kufanyika siku ya Jumanne.

Tume ya uchaguzi ya Zambia ilimtangaza Edgar Lungu kama mshindi wa uchaguzi wa rais kwa kupata asili mia 50.35 ya kura zote zilizopigwa, huku mpinzani wake Hakainde Hichilema, akipata asili mia 47.67 ya kura.

Kipengele kipya cha katiba kianamtaka mshindi wa urais kupata angalau asili mia hamsini ya kura zote, tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo mgombea angetangazwa mshindi akiwa na chini ya asili mia hamsini.

XS
SM
MD
LG